Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ukimtafuta Bwana Mungu wako utampata.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Tarehe: 16/10/2023.
Kumbu kumbu la Torati 4:29 “Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.”
Biblia inasema; “Kama ukimtafuta Bwana, Mungu wako, utampata,” Unampataje Mungu? Unampata pale ambapo Akili yako na Mawazo yako vinapokuwa na shauku, Moyo wako ukiwa na tamanio la kumtafuta ndipo utamuona. Biblia haikusema tumtafute Bwana kwa vinywa vyetu, la! Kwa maana tunajua sana kusema au kuomba lakini matendo na moyo vinakuwa tofauti.
Unapomtafuta Bwana unaweza usimuone kwa damu na nyama lakini anaweza kukujibu kwa ndoto au akamtuma hata mtu ili aseme na wewe; pale Akili yako, Mawazo yako na shauku yako vinapoungana kwa pamoja kumtafuta Mungu hakika utamuona.
Ondokana na kila jambo hasi akilini mwako linalomuhusu Mungu; usiwe na mawazo ya kusema; “Mungu ni Mtakatifu hivyo hawezi kunisikiliza mimi mwenye dhambi”, kama ukiwa na akili hiyo basi hautaweza kukutana naye. Unachopaswa kufahamu ni kuwa Mungu anaichukia dhambi lakini anawapenda wenye dhambi ili apate kuwasamehe, wakirejea Kwake anawasamehe. Mungu ni Mungu wa Rehema na ni Mungu wa Upendo pia ndio maana alimtoa Mwanawe wa pekee, alipitia mateso ili wenye dhambi waokolewe.
Hivyo Akili yako na Mawazo yako kwanza yatambue kuwa Mungu atakusikia na kukujibu ndipo uende mbele zake na kuomba na hapo ndipo utapokea majibu yako lakini ukiwa na akili kuwa wewe ni mwenye dhambi na Mungu hawezi kujibu maombi yako sahau kupokea majibu yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*