Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mapenzi ya Mungu kwa wamchao.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 24/10/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Zaburi 128:1-2 “Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.”
Siku zote ukimcha Bwana Yeye anakupa kuifurahia kazi ya mikono yako. Inawezekana katika maisha yako unapambana na kutaabika katika kufanya kazi usiku na mchana lakini hauifurahii pesa unayoipata kwa sababu inaliwa na matatizo au mazingira yanayo kuzunguka. Unaweza ukajikuta kila ukipata pesa ndipo matatizo yanaanza mpaka pale hizo pesa zitakapoisha, hilo sio kusudi la Mungu kwako.
Mungu anakupenda na anakuwazia mema siku zote na YEYE akikupa pesa ni ili uweze kuwa na maisha mazuri ili uweze kuufurahia Uumbaji wake. Ukiona unatumia nguvu kubwa kupata pesa lakini jasho lako anakula mtu mwingine, hayo siyo makusudi wala mapenzi ya Mungu kwako.
Wewe uliyemkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako (uliyeokoka) umebarikiwa katika Kristo Yesu, kwa Baraka zote za mwilini na rohoni. Hivyo basi kaa katika nafasi yako ili uweze kufurahia yale ambayo Mungu amekukusudia katika maisha yako. Ibilisi yeye ni muongo na ni mwizi, hana kitu chochote sasa akikuona wewe haujajitambua anaweza kutumia hali yoyote kuiba yale uliyokuwa nayo.
Ukiri:
• Baba yangu wa Mbinguni asante kwa Baraka zote ulizonibariki, nisamehe kwa kutokujitambua kuwa Mimi nimebarikiwa na hata nikasababisha ibilisi akachukua yale ambayo Wewe umenibarikia. Ibilisi wewe ni muongo na mwizi kuanzia sasa rudisha yale yote uliyoyaiba katika maisha yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*