Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Kama unataka kuchanua katika maisha yako mfanye adui yako awe majivu.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 25/10/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Kutoka 23:22b “Mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.”
Kuna mambo matatu ya msingi unapaswa kuyajua katika maisha yako wewe kama mwamini, kwa maana kamwe hautaweza kuchanua kama mambo haya yapo kwako:-
● Adui yako akiwa hai.
● Adui yako akiwa juu yako.
● Adui yako akiwa na wewe.
Je! Unatamani kupata yale ambayo Mungu amekukusudia? Usiwe rafiki wa adui zako, kwa maana Mungu mwenyewe amesema ” Mimi nitakuwa adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao.” Kama Mungu mwenyewe amesema kuwa YEYE atakuwa adui wa adui zako sasa Je! Wewe unakuwaje rafiki wa adui zako? Na YEYE amesema atakuwa mtesi wa hao wanaokutesa, Je! Wewe unakuwaje rafiki kwa wale wanaokutesa?.
Kama unataka kuchanua katika maisha yako wewe kama mwamini hakikisha adui yako anafanyika kuwa majivu. Usilale usingizi na kukoroma wakati yule anayekutesa halali usiku na mchana ili kuhakikisha anakuharibu, hakikisha unasimama katika nafasi yako ndipo utayaona yale ambayo umekirinimiwa na Mungu katika maisha yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*