Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mungu kamponya mume wangu ugonjwa wa akili

USHUHUDA
Naitwa Neema Joshua napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu. Ilikuwa ni siku ya tarehe 8 mwezi huu wa 10 siku ya mwisho ya kusanyiko kuu tulishiriki meza ya Bwana, mume wangu akaniambia amefurahi sana kushiriki meza ya Bwana na anahisi furaha moyoni mweke, tuliporudi nyumbani siku ya jumatatu tarehe 9 mume wangu alikuwa na furaha sana lakini gafla nikamuona kama hayuko sawa kama anachanganyikiwa, mpaka ilipofika jioni alikuwa amechanganyikiwa kabisa.
Tukampeleka hospitali ya Lugalo tulipofika akawekwa sehemu ya watu wenye matatizo ya akili; mume wangu alikuwa anavua nguo zote, watu wakienda kumuona anavua nguo zote, ile hali iliniumiza sana. Siku ya jumapili nikaja hapa kanisani nikamwambia Mungu “najua wewe unaweza haujawahi kushindwa na jambo lolote ninachoomba kwako ni mume wangu apone na kurudi nyumbani”.
Ilipofika siku ya jumatatu nilipoenda hospitali kumuona mume wangu, nilimkuta akiwa mzima kabisa na ameshuhudia watu habari za Yesu wodi nzima, mpaka madaktari wakaniuliza ninasali wapi, nikawaambia Efatha, akasema hakika Mungu wako anaweza, mume wako amepona usimuache Mungu. Namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu aliyonitendea mimi na familia yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*