Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ili ufanikiwe unahitaji kufahamu na kupenda kile unachokifanya

NENO LA SIKU.
Tarehe: 31/10/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Hapa chini ya jua yako mambo mengi sana usiyoyajua, lakini ili ufanikiwe katika jambo fulani lazima uwe na ufahamu nalo.
Huwezi kufanikiwa katika maisha yako katika jambo ambalo moyo wako na akili yako haulipendi, ili ufanikiwe katika jambo lazima kwanza ulipende hilo jambo. Usifanye biashara yoyote ambayo moyo wako haujaifurahia, kamwe hautafanikiwa. Usifanye kitu kwa sababu hauna jambo la kufanya, kwa maana ili ufanikiwe lazima ukipende kwanza kile unachokifanya.
Kwa kadri unavyofahamu mambo ndivyo utakavyofanikiwa na kustawi. Kwa jinsi watu wenye ufahamu walivyo wachache ndivyo waliofanikiwa na kustawi walivyo wachache huku duniani, kwa sababu ustawi wako na mafanikio yako unatokana na kile unacho kifahamu. Kupitia kile unachokifahamu kitakupa kufikia ustawi na mafanikio yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*