Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mshtaki mkuu.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 2/11/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
1 Petro 5:8-9 “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.”
Ibilisi ndiye mshitaki mkuu na wakati wote hachoki kutafuta ushindi. Hufanya hivyo maana alipoteza ushindi pale Kalvari miaka elfu mbili iliyopita. Ibilisi hatulii mahali pamoja, huzunguka zunguka na kutafuta jambo la kuwashitaki watu kwa Mungu.
Huwapa watu usingizi mzito na kuwaingiza katika kundi la wafu, ni muuaji na mwizi mzoefu. Yesu alimfananisha ibilisi na Mbwa mwitu aliye nyikani, ibilisi husababisha upofu, mtu asipate kuona anayopaswa kuona kulingana na Neno la Mungu.
Ili kumshinda ibilisi na asipate jambo la kukushitaki, tambua ngazi yako ya kupanda kufika juu. Usitamani kufika kileleni kwa lifti bali tumia ngazi na upande hatua kwa hatua. Weka malengo ya lini utafika wapi, usitamani kufika kileleni kama arukaye na ndege. Weka angalizo pekee kwa mshitaki wako ibilisi.Yesu alisema duniani kuna dhiki lakini hatuna budi kuishinda kwa sababu Yeye aliushinda ulimwengu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*