Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Neema ya kusikia

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 7/11/2023.
Ufunuo 6:22 “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
Mtu aliye na neema ya kusikia lazima atakuwa na neema ya kuishi, kusikia kunakupa kushinda; Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.”
Kusikia ni siri ya ushindi ukinyimwa kusikia basi umenyimwa kufanikiwa katika maisha yako kwa maana muujiza hautakuja hewani mpaka umesikia.
Ukisikia hata wasiokutamani watakutamani, waliokusukuma watakukumbatia, waliokudharau watakuheshimu na waliokukataa watakutafuta. Ukitaka maisha yako yabadilike muombe Mungu akupe neema ya kusikia.
Ndio maana unaweza kuona umesoma darasa moja na wenzako, wao wamefanikiwa lakini wewe unabaki kusema yule nilisoma naye, kwa nini kwa sababu mwenzako alisikia akaelewa na huko kusikia ndipo kukampa yeye kufanikiwa ila wewe ulikwama katika kusikia. Siku Mungu akikujalia kusikia taabu na maisha unayopitia itakoma. Amua sasa kusikia ili Mungu abadilishe uteka wako.
Muombe Mungu akupe kusikia na kuelewa kile ulichokisikia ili maisha yako yabadilike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*