Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Nguvu ya jina la Yesu

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 8/11/2023.
Waebrania 2:3 “ Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”
Injli ni uweza wa Mungu sio uweza wa wanadamu au uweza wa dini bali ni uweza wa Kiungu, tunaposema Injili maana yake ni Jina linalopita majina yote linahubiriwa.
Siku moja kulikuwa na kiwete ambaye anakaa katika lango la mji ili aombe, kila mtu wa mji ule alijua habari za huyo kiwete na kila aliyepita alimpa kitu, siku moja Petro na Yohana walipokuwa wakipita, yule kiwete alitarajia kupokea kitu kutoka kwao lakini Petro na Yohana wakamwambia, “pesa na dhahabu hatuna ila tunakupa tulichonacho, kwa JINA LA YESU inuka uende.” Yule kiwete akaamka na kutembea; yule kiwete alitarajia kupata fedha lakini akapewa UZIMA na akatembea mwenyewe.
Matendo ya Mitume 4:7b “Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya?”
Ili mambo yatokee katika maisha yako lazima uwe na mambo mawili tu:
• Una Jina la nani.
• Una Nguvu gani unayotembea nayo.
Mchawi yeyote haogopi jina bali anaogopa Nguvu iliyopo ndani ya hilo Jina, ukiwa na Jina lenye Nguvu unapolitaja hata mapepo yanakimbia.
Kupitia JINA la YESU miujiza inafanyika, kazi ya Jina katika ulimwengu wa roho ni kuumba miujiza na kazi ya Nguvu ni kushinda pingamizi yoyote inayokuwa kinyume na hilo Jina. Ukikubali kuwa na Jina la YESU hakuna kitakachokushinda katika ulimwengu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*