Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Amepona kifafa kwenye maombezi katika mkutano wa sifa Mererani..

USHUHUDA:
Naitwa Musa Kibure, napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, nilipata tatizo la kifafa ukubwani, tatizo hili lilinianza siku moja usiku niligongewa mlango na majirani nakupewa taarifa za msiba ndipo nikapoteza fahamu. Tatizo hili likaendelea siku baada ya siku, ilikuwa kila ikifika tarehe 28 na 30 lazima nianguke kifafa na hali hiyo ilikuwa inanikuta wakati wa usiku, ambayo asubuhi yake ni siku ya mnada na mimi nilikuwa ni mfanyabiashara wa mbuzi pamoja na ng’ombe mnadani; kwa sababu hiyo nilishindwa kabisa kufanya biashara zangu, hali iliyonipelekea kuwa na madeni mengi sana. Nimehangaika na hali hiyo kwa muda wa miaka mitatu. Napenda kumshukuru sana Mungu kwa ajili ya mkutano wa Sifa Mererani, nilihudhuria siku zote na niliombewa, sikuweza kushuhudia kuwa nimepona kwa kuwa nilikuwa nasubiri tarehe za kupata kifafa zifike ili nithibitishe ushuhuda wangu.
Namshukuru sana Mungu kwani tangu mwezi wa nane mpaka leo hii mimi ni mzima kabisa sikuwahi kuanguka kifafa baada ya ule mkutano. Namshukuru sana Mungu Yeye awezaye kufanya mambo yote ambayo wanadamu wameshindwa kwa maana nimehangaika sana mahospitalini kwa muda wa miaka yote hiyo mitatu lakini sikupokea uponyaji wangu; namtukuza sana Mungu kwa matendo yake makubwa aliyonitendea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*