Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mruhusu Yesu aingie moyo

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 20/11/2023.
Ufunuo 3:20-22 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
Yesu anasema “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha” Mlango huu unaozungumziwa hapa sio ule wa nyumbani kwako, chumbani kwako, jikoni kwako, ofisini kwako au mlango wa gari yako, la! Bali ni Moyo wako; ukiufungua Moyo wako Kwake Yeye ana uwezo wa kuingia ndani yako na kubadilisha mambo ndani yako. Anaweza kuingiaje kwako? Mungu ni Roho na Roho ina uwezo wa kuingia kwa mtu kwa maana mtu pia ana roho.
Kwa nini anataka aingie ndani yako? Kwa sababu ndani ya mtu kuna vurugu nyingi, Biblia inasema “moyo una ugonjwa wa kufisha” kufisha maana yake ni kuua. Una nini Moyoni mwako wewe? Hicho kilichopo Moyoni mwako ndicho kinaamua kesho yako iweje, uishije na familia yako, watoto wako au mume au mke wako, hicho kilichopo Moyoni ndicho kitaamua afya yako iweje, kama kilichopo Moyoni hakina nguvu ya Kiungu matokeo utayaona katika mwili ndipo unaona magonjwa na masumbufu ya kila aina.
Ukimruhusu Yesu aingie na akae Moyoni mwako magonjwa, umaskini, aibu, misiba na kushindwa havitaonekana kwako kwa sababu Yeye ni mshindi alishinda kifo na mauti hivyo na wewe utashinda kila changamoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*