Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Bila Yesu huwezi jambo lolote

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efath.
Tarehe 23/11/2023.
Yohana 15:5 “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya jambo lolote”.
Mwana wa Mungu unapaswa kutambua kuwa bila Nguvu ya Mungu hauwezi kitu katika maisha yako.
Yesu yupo anakuita anataka umtumikie, anataka uwe wa Kwake. Achana na mambo ya zamani mgeukie Yesu na Yesu atakuweka huru maana Yeye amesema, katika Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”
Kwa nini unaendelea kuumia na kuteseka? Ni kwa sababu hauko tayari kufanya kile Mungu anachotaka, hauko tayari kumpa Yesu maisha yako na kuruhusu kuongozwa na Roho Mtakatifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*