Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Siku zote tamaini kuwa mwanafunzi

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Tarehe 24/11/2023.
Mathayo 28:19 “19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;”.
Bwana YESU aliwaambia Wanafunzi wake enendeni, mkawafanye Mataifa yote kuwa Wanafunzi, hakusema nendeni mkawafanye kuwa madaktari, au wachungaji, Wanafunzi siku zote wanapenda kujifunza ili waweze kufaulu vyema.Yesu alituita sisi tuwe Wanafunzi wake na siyo wafuasi wake, wakristo wengi wanataka kuwa wafuasi na siyo Wanafunzi.
Uanafunzi ni wito wa juu katika Kristo. Kabla haujapitia chochote tamani kuwa Mwanafunzi wa YESU hii itakusaidia kuyashinda majaribu. Hata kama unataka kuoa au kuolewa jifunze kuwa Mwanafunzi, yaani tamani kujifunza vitu vipya kila iitwapo leo kwa ajili ya ndoa yako. Mke unayemuoa ametoka aina fulani ya maisha na wewe umetoka katika aina nyingine ya maisha hivyo mnahitaji kujifunza ili muwe kitu kimoja kama sivyo mtaishia kupeana talaka.
Vivyo hivyo katika biashara lazima ushinde, wengi wenu mmeshindwa biashara kwa sababu ya kushindwa kuwa Wanafunzi hautaki kujifunza. YESU hafurahishwi na kushindwa kwako. Ili uweze kufika mahali ambapo unataka kufika ambapo utaziona baraka zako ni lazima ukubali kujifunza.
UKIRI.
Kuanzia leo nitatumia muda wangu Kujifunza na kutafuta Maarifa zaidi juu ya Biashara yangu, Ndoa yangu, Utumishi wangu na Kazi yangu ili niweze kuwa Mtu Mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*