Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ushuhuda

Naitwa Lucy Nicetus, namshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu kwangu, kwanza napenda kumshukuru sana kwa kutimiza miaka 13 ya wokovu na miaka 23 ya ndoa yangu.
Pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuniponya, siku moja nilianguka na pingili za mgongo zilisagika, hali hiyo ilinipelekea kupata maumivu makali sana ya mgongo na hata kushindwa kutembea, ndani ya miezi miwili nililala kitandani siwezi kutembea, ilipofika kipindi cha kwenda kusanyiko nilimwambia Mungu sijui itakavyokuwa lakini mimi naenda. Namshukuru sana Mungu baada ya kusanyiko la mwaka huu mwezi wa kumi na kurejea nyumbani nikaanza kupata afya nzuri na sasa natembea vizuri kabisa bila maumivu yoyote.
Lakini pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa kutimiza miaka 13 ya wokovu na kupitia wokovu wangu nimemuona Mungu akifanya mambo mengi sana katika maisha yangu. Niliokoka nikiwa sina nyumba lakini mpaka sasa nina nyumba mbili na nina usafiri. Hakika kumtumikia Mungu kuna faida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*