Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ushuhuda

USHUHUDA:
MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA
Mimi pamoja na mke wangu tunapenda kumshukuru sana Mungu kwa kutujalia kutimiza miaka 30 ya NDOA. Mungu amekuwa mwema sana kwetu kila iitwapo leo na ameyafanya maisha yetu kuwa baraka kwa wengi.
Kuachana ni jambo baya sana lakini kupendana ni kuzuri. Ili muweze kusameheana na kuchukuliana; upendo unahitajika, bila upendo kamwe hamtaweza. Ukiona mtu hawezi kusamehe fahamu kuwa hana upendo.
Mungu ni pendo na ukiona mtu anasamehe fahamu kuwa anaupendo na kama anasamehe jua kuwa ana Mungu. Ukiona mtu ameshindwa kusamehe jua kuwa hana Mungu na kama hana Mungu basi hana pendo.
Mimi sijuti na sitajuta kuwa na mke wangu mzuri Eliakunda, mke wangu asipokuwa nyumbani najikuta kama nimepungukiwa kitu na sahau kutandika kitanda, kula na hata kuoga, sijajua kama nyie wanaume mliooa kama wake zenu ni wazuri kama wangu, mimi sijui, ila wa kwangu ni mzuri. Ndoa ni ibada kama unavyoshiriki meza ya Bwana na kuiheshimu basi heshimu ndoa yako. Mungu anachukia kuachana, kushikilia mambo moyoni inachagia kuachana, watu wawe na presha na hata kisukari. Asante mke wangu Eliakunda kwa kunitunza na kunipenda.
Maombi kwa wababa:
Bwana Yesu nipe kuwa na pendo ndani yangu, nimpende mke wangu, nimlee na kumtunza siku zote za uhai wangu asisikie kujuta kuwa na mimi.
MAMA ELIAKUNDA MWINGIRA:
Mungu ni mwema sana, namshukuru Mungu kwa pendo lake na fadhili zake kwetu mpaka kufikia siku hii ya leo tumefikisha miaka 30 ya ndoa.
Namshukuru sana Mungu kwa kunipa mume mzuri anayenipenda na kuniheshimu. Kitu kinachofanya watu wawe pamoja ni upendo.
Wengine wanapokaa miaka mingi wanachokana, mwanangu Mungu asikupe kumchoka mwenzi wako, kama mlianza katika pendo maana pendo halihesabu mabaya halijivuni na halikosi kuwa na adabu. Mungu akupe neema ya hilo pendo.
Nawatakia wote mlioolewa mkawe na maisha mazuri ya ndoa na wale ambao hamjaolewa Mungu akawape wenza sahihi na mkafurahie maisha yenu ya ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*