Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Yesu alipitia mateso ili sisi tuwe na furaha

Watch Now

Download

Yesu alipitia mateso ili sisi tuwe na furaha

ASKOFU THABO MASENYA KUTOKA AFRIKA YA KUSINI:
Zaburi 30:11 “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.” Watu wengi wanapitia katika magumu au mabaya lakini huo sio mpango wa Mungu; kila aina ya ubaya, huzuni au maumivu uliyokutana nayo acha Bwana akayaondoe na akuletee furaha na mashangilio katika maisha yako.
Neno la Mungu linasema “Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;” Katika matanga yoyote uliyokutana nayo katika maisha yako Mungu akalete mazuri kwako.
Biblia inasema kuwa “Bwana hufurahia katika ustawi wa watumishi wake” Mungu anafurahia ustawi wa watumishi wake, ustawi wowote utakaokutana nao fahamu kuwa utamfurahisha Mungu, Mungu kamwe hafurahii unapoteseka, Bali anafurahi pale ambapo wewe unastawi.
Ibilisi amewaaminisha wengi ya kuwa kumtumikia Mungu ni mateso, lakini Biblia inasema kuwa “Yesu alipitia mateso ili sisi tuweze kuwa na furaha” Ni mapenzi ya Mungu juu yako ya kuwa upitie katika mazuri na ustawi na siyo magumu. Mungu anataka upitie katika ustawi na siyo umaskini, nia ya Mungu katika maisha yako ni kwamba uweze kuona mazuri yake mahali unapoishi na sio kupitia katika maumivu na huzuni.
Hakuna sababu ya wewe kusherekea ustawi wa Mungu utakapofika mbinguni, la! Bali utafurahia hapa hapa duniani kwa maana Yesu amekwisha kulipa gharama yake ili wewe uishi maisha mazuri huku duniani.
Kama ustawi wako umeshikiliwa kuzimu, leo Baba yangu wa mbinguni akakufanye ukawe huru kutoka katika kila mtego wa ibilisi; kwa maana sio mpango wa Mungu wewe ung’ang’ane; acha baraka za Mungu alizokuwekea zikafunuliwe kwako kwa Jina la Yesu na ukazifurahie.