Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Pasipo Mungu sisi hatuwezi

NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
Tarehe 12/12/2023
Mithali 16:3 “ Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika.”
Katika dunia hii, sisi wanadamu mara zote tunafikiri kuwa tunaweza kufanya kila kitu kwa nguvu na uweza wetu, lakini ngoja nikwambie kuwa hauwezi kufanya lolote kwa nguvu zako. Wakati mwingine tunaonyesha uwezo, nguvu, maarifa na ujuzi wetu, lakini unapaswa kutambua kuwa pamoja na wewe kuwa na hivyo vyote pekeyako hauwezi na ndio maana Yesu akasema “pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya lolote”.
Namna unavyoamka asubuhi, unavyozungumza na kutembea ni nguvu zake ndizo zinazokuwezesha wewe kufanya hayo. Ndio unaweza kusema kuwa unaweza, lakini ngoja nikwambie, katika uzoefu wangu mimi wa kumjua Mungu mwanadamu hawezi kufanya lolote isipokuwa Mungu amemuwezesha kufanya.
Wakati mwingine tunadhani kuwa tunaweza lakini unapaswa kutambua kuwa pasipo ruhusa yake hauwezi kuamka asubuhi. Ukitembea, ukila, ukipumua usijeukasema ni kwa nguvu zako, la! Bali ni kwa nguvu zake tu.
Lolote ulitendalo huku chini ya jua kama unataka litimie unapaswa kutambua kuwa pasipo Mungu wewe hauwezi lolote, haijalishi una fedha kiasi gani za kutimiza hilo jambo lakini pasipo Mungu hauwezi.
Mwanadamu ukila ukashiba acha kuwa na kiburi, mkumbuke Mungu wako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*