Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Usikubali kitu chochote kikubadilishe imani yako

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josepat Elias Mwingira Kanisa la Efatha.
Tarehe 13/12/2023
1 Wafalme 18:43-44 “Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.”
Elisha baada ya kuomba kwa ajili ya mvua alimtuma mtumishi wake Gehazi akaangalie kama kuna mawingu ya mvua lakini akarudi na kumwambia Elisha hakuna kitu; Elisha hakubadilisha maombi bali aliendelea kuomba mpaka mvua ilipotokea.
Watu wengi leo hii wanashindwa kupokea yale waliyoyaomba kwa Mungu kwa sababu baada ya kuona wameomba kwa kitambo na majibu hayajatokea wanabadilisha maombi yao. Mwana wa Mungu ili uweze kupokea kutoka kwa Baba yako wa mbinguni kile ulichomuomba, hakikisha usibadilishe kauli mpaka imekuwa sawa sawa na vile ulivyoomba. Usibadilishwe na mtu, hali wala mazingira hakikisha unasimamia kile ulichokiomba mpaka kinakuwa.
Usikubali kitu chochote kibadilishe Imani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*