Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Kubali kufundishwa

NENO LA SIKU

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha

Tarehe 14/12/2023

 

Daniel 1:15 “Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.”

Unaposikiliza mashauri unayopewa ndivyo unavyokuwa bora kuliko wenzako. Daniel na wenzake walikubali kuongozwa na Roho na wakaamua kuyasikiliza mashauri yake na akawafanya kuwa bora kuliko wengine. Kwa nini upo hivyo ulivyo leo? Ni kwa sababu hausikilizi mashauri unayopewa. Unakuta mtu anakwenda Kanisani anafundishwa na kupewa mashauri lakini akitoka kanisani hafanyii kazi kile alichofundishwa.

Unakuta mtu ni mzuri sana kuhudhuria Kanisani kila Jumapili au Semina lakini yupo hivyo hivyo miaka yote, kwa nini? Kwa sababu hafanyii kazi kile anachofundishwa, halafu anasema yupo na Mungu, la! Usijidanganye, fahamu kuwa uko wewe mwenyewe, hauko na Bwana wa mabwana. Kama upo na Bwana wa mabwana na unatendea kazi mafundisho yake unayopewa na watumishi wake kamwe hayo mafundisho hayata kuacha uwe kama ulivyo bali yatakubadilisha.

Unachukuaje mambo ya rohoni na kuyaleta katika ulimwengu huu wa kawaida? Kwa kukubali kukitendea kazi kile ulichokisikia yaani mafundisho unayopewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*