Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mahubiri Ibada ya Jumapili 31/12/2023

Watch Now

Download

Mahubiri Ibada ya Jumapili 31/12/2023

Tangu mwaka umeanza tumekuwa tukisikia shuhuda nyingi kwa watu mbali mbali, kwa maana hiyo kama haujapokea chochote kutoka kwa Mungu jua kuwa haujampenda kwa maana wapendanao wanapeana zawadi, kama unampenda Mungu lazima atakutendea miujiza. Kama haujaona tendo lolote kutoka kwa Mungu basi haujampenda, kwa maana hata kupumua, kutembea, kupata chakula pia ni pendo la Mungu. Wasiopendwa hata kutokea duniani hawatokei wanaishia tumboni lakini wewe na mimi Mungu amependa tuwepo ndio maana tunapumua ni kwa sababu ya Pendo la Mungu kwetu.

1 Yohana 3:1-3 “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.”
Kwako wewe uliyeokoka hongera kwa maana umefanywa kuwa mtoto wa Mungu, Biblia inasema “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo.” Kwa maana kuanzia saa ile ulipoitwa mwana wa Mungu (siku ulipookoka) ukoo wako ulibadilishwa, siku ukielewa hilo njaa haitakusumbua, magonjwa hayatakutesa wala umaskini hautakushikilia kwa maana wewe ni mwana wa Mungu na kitu chochote kilichoumbwa na Mungu lazima kikusalimie kwa maana wewe ni mwana wa Mungu.
Wewe uliyeokoka umefanyika kuwa mwana wa Mungu, sasa unalia lia nini? Wakati wewe ni mwana wa Mungu na haujaomba uwe mwanaye bali Yeye Baba wa Mbinguni amekufanya kuwa mwanaye kupitia Yesu Kristo, jitambue na usimame katika nafasi yako nawe hautakuwa kama ulivyokuwa.
Kuanzia siku ile tangazo lilipotoka kuwa wewe ni mwana wa Mungu chochote ambacho umetamkiwa ni chako.
Waefeso 1:3-4 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.”
Wewe ulichaguliwa na Mungu uwe wa kwake kabla bahari haijatengwa, anga halijatengwa, wanyama hawajaumbwa; kabla baba na mama yako hawajatokea katika ulimwengu huu. Wewe ulichaguliwa kwamba utazaliwa katika tumbo la mama yako ili uwe mwana wa Mungu.
Biblia inasema “kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” Ni kweli umezaliwa na mama aliyekuzaa, wewe hauna hatia, ulipita katika tumbo la mama yako na viuno vya baba yako ili ufike siku hii ya leo uitwe mwana wa Mungu.
Yale yote yanayotoka upande wa baba yako au upande wa mama yako leo ni mwisho, kwamba walitumia njia gani wewe uwepo, Mungu aliwaridhia na akawatumia ili kukuleta duniani. Haijalishi kwamba walikunywesha miti shamba au walikuchanja chale lakini Mungu alikuridhia uwepo duniani.
UKIRI:
Leo Baba yangu wa Mbinguni mimi nimeokoka na nimeelewa kuanzia leo naanza safari yangu nikiwa nimeichukua DNA yako maana mimi ni mwanao.
Usioe au kuolewa na mke au mume kwa sababu unataka vitu vya mserereko. Mke mwema hatoki nyumbani kwa baba na mama yake bali ni yule anayetoka kwa Bwana, na ukipata mke atokaye kwa Bwana, hautakufa maskini lazima utaenda hatua kwa hatua, na mara zote mke anayetoka kwa Bwana hatapenda wewe uaibike bali atakuwa akikushauri nini cha kufanya ili uzidi kung’aa mbele za Bwana. Muombe Mungu akupe mke mwema.
Mke mzuri atokaye kwa Bwana ndio kioo chako na ni mshauri wako, ndio maana Biblia inasema “apataye mke amepata kitu chema” mimi sijui wewe wa kwako umempata wapi. Lakini huyo ni zawadi yako kutoka kwa Bwana chochote akisema inamaana kuwa ametoa kwa Bwana na ukikikataa inamaana kuwa umemkataa Bwana na ukikisikiliza ndivyo unavyoponyeka.