Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Ushuhuda

Naitwa Nuru Mtoi, nilikaa muda mrefu bila kupata kazi, ilipofika mwaka 2020 niliweza kupata kazi na kufanya kwa muda wa miaka mitatu nikiwa kama kibarua na mwaka huu kampuni ilitangaza kufungwa hivyo sikuwa na stahiki zozote kama mfanyakazi kwa sababu nilikuwa sijaajiriwa . Baada ya kampuni kufungwa walioajiriwa walilipwa vizuri na ndipo muajiri wangu aliponiuliza anifanyie nini, moyoni mwangu niliwaza kiwango cha pesa lakini nilipoomba nikamshirikisha Roho mtakatifu, niliambiwa niombe waninunulie nyumba, niliporudi na kumwambia mwajiri wangu alikubali na kweli nikapata nyumba nzuri kwa bei nafuu na sasa namiliki nyumba yangu ipo Kerege, Bagamoyo ina vyumba vinne vya kulala.
Hakika namshukuru Mungu wa Efatha, mimi kumiliki nyumba ni neema iliyopitiliza. Pamoja na haya yote nimemaliza kulipa nadhiri yangu ya ujenzi wa kanisa, namshukuru sana Mungu na watumishi wake kwani wamefanyika msaada mkubwa kwenye maisha yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*