Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

MUNGU ANAKWENDA KUONDOA KIZUIZI CHAKO ILI UPATE KUMILIKI.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 10/1/2024.
Mwanzo 32:28 “Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.”
Mungu alimbadilisha Yakobo jina na kumuita Israeli lakini hakuweza kuitwa hilo jina kwa sababu kulikuwa na kizuizi katikati ambaye ni Raheli, hivyo Yakobo hakuweza kutimiliza wito wake kwa sababu ya hicho kizuizi. Baada ya Raheli kufa ndipo watu wote wakaanza kumuita Yakobo Israeli; kwa nini? Kwa sababu kizuizi kimeondoka.
Sijui ni nani au kitu gani ambacho ni kizuizi katika maisha yako ambacho kinakufanya wewe ushindwe kutimiza mapenzi ya Mungu, ila tambua Mungu anakwenda kukiondoa. Kamwe Mungu hatakuacha ushindwe kutimiliza wito wako bali ataondoa hicho kizuizi, katika Mwaka 2024 Utamiliki Milki yako.
Daudi aliitwa lakini hakuweza kutembea katika wito wake kwa sababu kulikuwa na kizuizi ambacho ni Sauli, Mungu akashughulika na Sauli ili Daudi aweze kutimiliza wito wake.
Mwanangu kizuizi chochote kilichopo katika maisha yako, Mungu akakiondoe sasa ili uweze kumiliki milki yako katika Mwaka huu wa Kumiliki na kisiwepo cha kukuzuia wewe ushindwe Kumiliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*