Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

NAMNA YA KUTAWALA NA KUMILIKI KWA MAMLAKA TULIYONAYO

MCHUNGAJI ELIZABETH NGAINA
Mwanzo 1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.”
Mungu alipomuumba mtu ndani yake aliweka mamlaka na uwezo wa kumiliki, lakini mwanadamu alipoteza ile mamlaka ya umiliki wake kwa sababu ya dhambi. Mungu alimtuma Yesu Kristo ili kuirejesha hiyo mamlaka kwa kila atakayemwamini.
Unapomwamini Yesu Kristo kuna mamlaka inaachiliwa kwako na kuruhusiwa kutembea na wewe, itakuongoza na kukuelekeza kwa sababu tayari umekwisha kumwamini mwana wa Mungu. Yohana 1:12 ” Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” Unapopewa uwezo inamaana kuwa umerejeshewa mamlaka yako kwa sababu wewe ni mwamini. Je! Wewe unaamini?
Jamii kubwa ya waliookoka (waamini) wanayo ile mamlaka ya kumiliki lakini hawaitumii hivyo huishia kuangamia au kuangamizwa. Hosea 4:6a “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”
Umiliki unatakiwa kuanza na wewe, kwanza unatakiwa ujitambue kuwa wewe ni mmiliki, Yapaswa umiliki mambo yafuatayo:
• Afya yako
• Uchumi wako
• Ndoa au uzao wako
• Hisia na mawazo yako,
Usipoweza kujimiliki mwenyewe ni hatari sana kwa sababu hautaweza kufikia ile hatima ambayo Mungu amekwisha kukuandalia.
Umiliki unahitaji nidhamu; Lazima uwe na nidhamu katika kile ambacho umekipata. Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.” Kuna mahali Mungu ametuandalia, mahali pa umiliki wetu lakini panahitaji adabu ili uweze kumiliki.
KANUNI ZA UMILIKI:
1. Utii; ili uweze kumiliki lazima umsikilize yule aliyeko mbele yako, lazima uwe mtii kwa baba yako wa kiroho. Yoshua 1:7 “ Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.”
2. Kuishi maisha matakatifu; utakatifu ni tabia ya MUNGU; Mithali 8:20-22 “Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao. Bwana alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake, Kabla ya matendo yake ya kale.”
ukitembea katika utakatifu yale mazuri yote ni halali yako kuyapokea.
3. Ujasiri; ujasiri ni uwezo wa kufanya vitu vingine ambavyo mtu mwingine anaviogopa kuvifanya, ujasiri ni kiwango cha kuwa na uthubutu kinachokupa kutenda bila hofu.
• Ujasiri ni uwezo chanya au postivu unakupa kuona kwamba unaweza kufanya vitu ambavyo wengine hawawezi.
4. Tumia muda wako vizuri; Waefeso 5:15-16 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.”
• Mafanikio yetu yamefungwa ndani ya muda hivyo matumizi sahihi ya muda yatakupa kumiliki kwa urahisi kwa sababu kwa kila jambo chini ya jua kuna umiliki wake
5. Weka lengo la kile unachotaka kukifanya;
Elewa nini unapaswa kufanya ndani ya muda sahihi, hakikisha malengo yako yanatimia wala usiyumbishwe na chochote.
6. Kubali kuwa mtu wa kutatua changamoto na sio kuzikimbia. Kama Biblia isemavyo “Duniani mna dhiki lakini Kristo alikwisha kutushindia hivyo tembea ukijua wewe ni mshindi kwa kila jambo lolote litakalokujia.”
UKIRI:
Kuanzia leo wewe macho yangu ukatazame yale yote yatamanikayo na yenye thamani, na masikio yangu kuanzia leo ukasikie sawa sawa na umiliki wangu, ee kinywa changu ukakiri sawa sawa na jinsi macho yalivyoona na masikio yalivvyosikia kwa habari ya kumiliki kwangu.
Eeh! Miguu yangu unipeleke kwenye umiliki wangu sawa sawa na Yoshua 1:3 “Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.” maana popote utakaponipa kupakanyaga umenipa. Akili yangu ukanipe kufanana na chochote ambacho kitakachonipelekea kwenye umiliki wangu.
MAOMBI
1. Muombe Mungu akupe akili yake ili uweze kufikiri na kuwaza kama Yeye.
2. Muombe Mungu aachilie mamlaka yake kwetu leo hii ili tuweze kumiliki milki zetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*