Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SEMINA YA UMILIKI – MAMBO YANAYOWEZA KUKUZUIA USIMILIKI

SEMINA YA UMILIKI – KANISA LA EFATHA MWENGE
MCHUNGAJI: CAROLINE SIGONDA
Huu ni mwaka wetu wa kumiliki. Tangazo limetolewa kwamba twende tukamiliki. Tangazo hili linaonyesha kwamba kanisa tayari limeshafunguliwa na liko huru kumiliki maana ni utaratibu wa Mungu kumilikisha watu waliowekwa huru maana anajua hawataibiwa tena.
Kwanza kabisa elewa kwamba Mungu ameridhia wewe umiliki na kutokumiliki kwako hakuhusiani na Yeye kabisa.
Hesabu 13:26-33 “Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.…….”
Mambo yanayoweza kukuzuia usimiliki:
1. KUKOSA MAONO
• Je! Una maono gani juu ya kile unachotaka kumiliki? Mungu anaweza kukuonyesha jambo lakini kwa kukosa maono ukakataa kupokea kwa kukosa ufahamu na mwisho ukaishia kukosa kile unachokitaka na ukaishia kuangamia. Joshua na Kalebu waliona maono ya nchi ya ahadi, wakaamini alichosema Mungu kwa Mtumishi wake Musa na ndio maana waliweza kuleta taarifa nzuri kwa Musa. Wenzao walienda, hawakuona nchi kama ni nzuri na hivyo walikataa kukubaliana na Mungu. Walileta habari za uongo kwamba nchi inawala watu huku wao wenyewe wakiwa wamerudi wote wazima.
• Je! Umeamini huu ni mwaka wa kumiliki? Je! Umechukua muda wa kuona alichokuahidia Mungu mwaka huu ili kukiendea? Je! Umekubaliana na ahadi ya Mungu? Ni vizuri ukakubali kuongozwa na Roho wa ufahamu ili kujua namna ya kuiendea Milki yako.
Ukiona Milki yako hutapoteza muda na mambo ya ulimwengu, utakuwa makini mno ili usipishane na Milki yako.
2. MANUNG’UNIKO /MALALAMIKO
Mara zote unapokuwa unakaribia kumiliki au kukipata kile Mungu amekukusudia, kuna habari huwa zinatokea halafu unaishia njiani. Wakati unapokaribia kumiliki ni rahisi sana kujaribiwa na mazingira ukaanza kunung’unika. Wana wa Israeli walipokua wanaelekea kuingia nchi ya ahadi walipokea taarifa ambazo zilisababisha wanung’unike na kushindwa kuingia kwenye nchi ya ahadi, manung’uniko yanaweza kukuondolea muujiza wako.
• Wanung’unikaji ni watu ambao hupenda kutafuta sababu ya kutofanya jambo, wavivu, wanapenda kulaumu, hawana shukrani, wakosoaji n.k; watu hawa ni wale ambao hawapendi kutii maagizo. Cha ajabu watu hawa ni wazuri sana katika kuhudhuria ibada, hawakosi ibadani, mikesha, zoni, kambi, kusanyiko, waombaji wazuri na hauwezi kuwatambua kwa sababu wako kila mahali.
Unapoelekea kumiliki angalia sana mazingira yasikuvuruge ukashindwa kupokea milki yako.
3. KUTOKUBADILISHA NAMNA YA MAOMBI
• Lazima mwaka huu uombe kama mtu anayejua anachofanya. Wakati mwingine watu wana maombi yanayoonyesha kutokuelewa haki yao na ndio maana hawawezi kupokea. Maombi ya mwaka huu yawe ya ufahamu. Omba sana Roho wa ufahamu akuongoze namna ya kuomba.
Tangazo limetoka nenda kamiliki sio omba ukamiliki.
Huu ni mwaka wa kutamka, acha kwenda mbele za Mungu huku unalia bali tangaza kwa maana tayari umeshapewa kumiliki. Maombi yako utakapoyabadilisha ndipo Roho Mtakatifu atakuongoza kumiliki hicho kitu, omba maombi ya ufahamu.
4. KUKOSA UHODARI, USHUJAA NA UJASIRI
• Mahali popote penye milki yoyote kumbuka kuna mtu anayeimiliki tayari; unatakiwa umuondoe, kuna mpambano ambao unahitajika hivyo uwe hodari ili kumuondoa ili uweze kumiliki. Nchi ya Kaanani ilikuwa ina watu wanaishi tayari, Ilibidi Joshua kupitia uhodari wake ajidhatiti ili kuingia katika nchi Ile. Kumbuka adui alishavamia na ni king’ang’anizi, hivyo inahitajika nguvu na ujasiri wako wa kukiri ili kile ulichotangaziwa uweze kukimiliki.
5. KUKOSA UZINGATIVU WA MAAGIZO:
• Wakati mwingine kuna ushindi tunaupata wa kumiliki kwa kuzingatia maagizo tu. Hakikisha mwaka huu unafanya kile unachoagizwa na utaona usaidizi katika kumiliki kwako. Yoshua aliangusha kuta za Yeriko kwa kufuata maagizo tu.
• Nehemia alizingatia lengo na kusudi lake; hata pale watu walipotaka kumpotosha hakulegeza kamba aliendelea na kusudi lake. Usikubali kupotoshwa na jambo lolote; usianze kuzunguka kwenye maombi maana utapokea neno tofauti na mwisho ushindwe kumiliki. Tulia mpaka kieleweke
Ukizingatia maagizo mwaka huu kuna muda mwingine hautahitaji kupigana bali Mungu atakupigania.
6. KUKOSA UVUMILIVU JUU YA KUMILIKI
• Elewa tunatofautiana vitu vya kumiliki. Kama umeomba maombi ya vitu ambavyo vinachukua muda mrefu kutimia acha kujipa msongo wa mawazo. Wapo wengi wanapoona wenzao wamepokea milki yao wanaanza kuona kama Mungu amewaacha.
Mfano: Mchicha na Mti wa Machungwa. Usionee wivu mtu anayevuna mchicha wakati wewe umepanda Mchungwa. Mtu aliyeomba milki ya mchicha na mti wa Machungwa muda wa mavuno unatofautiana. Aliyeomba mchicha atavuna na baada ya muda mfupi anaanza kupanda tena; lakini mchungwa unachukua muda ila ukianza kuvuna hanahaja ya kupanda tena bali kila mwaka atakuwa anavuna.
Elewa Milki yako na uwe mvumilivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*