Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

NENO LA SIKU

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.

Tarehe 17/01/2024.

Wapo watu walipookoka walipata mpenyo na kusikia sauti ya Mungu, lakini baadae hawamsikii tena kwa sababu ya kujichanganya kwao ambapo Pendo la Mungu lilipungua kwao. Unapokosa kusikia sauti ya Mungu unasikia sauti ya roho zidanganyazo na mwisho wake unakufa kifo kibaya cha kiroho, kwa kukosa kuelewa ulikotoka, uliko na unakokwenda. Unapokosa kusikia sauti ya Mungu, unakosa pia usaidizi wa Mungu na unapomlilia ili akutetee katika jambo fulani, hupati utetezi wowote.

Mithali 1:24-26″ Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu; bali mmebatilisha shauri langu, wala hamkutaka maonyo yangu; Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, nitadhihaki hofu yenu ifikapo;”

Usikubali Mungu akae pembeni na kukucheka siku ya msiba wako. Kuna watu ambao Mungu anawakataza jambo, lakini kwa sababu wanawaogopa watu au wana maslahi yao binafsi, wanaendelea kufanya. Hali hii ikiendelea uwepo wa Mungu unaondoka kwako, mambo yanakuwa magumu, mabaya yanakupata na yanakuwa vigumu kuondoka kwako. Amua kubadilika pale unapoonywa kuhusu tabia au jambo fulani ili usiingie katika hali ya majuto baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*