Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

TABIA INAWEZA KUSABABISHA USIMILIKI.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Tarehe 22/1//2024.
Mwanzo 4:6-7 “BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”
Hapa tunaona Mungu akimwambia Kaini, “kwa nini una ghadhabu?” Inamaana kuwa ile hali ya ghadhabu aliyokuwa nayo Kaini ilikuwa ikimvutia ibilisi kumkaribia. Safari ya maisha ya mtu anayetamani kumiliki ana mpambano kati yake na dhambi, dhambi ambayo inamkaribia kwa sababu ya tabia zake. Mungu anatamani moyo wako umkaribishe, huku ibilisi anahitaji tabia yako mbaya ili apate kukukaribia.
Mabadiliko ya tabia yatakupelekea uwe masikini au tajiri, mchawi au mtakatifu, tabia haina umri wala imani, unaweza ukawa na imani lakini tabia yako inasababisha uwe uliyeshindwa, unaweza ukawa hauna imani lakini tabia yako itamfanya Mungu akushindie. Ili uweze kupokea baraka kutoka kwa Mungu badili tabia yako itakayokufanya wewe uweze kuwa na Imani ili uweze kupokea Baraka kutoka kwa Mungu.
Musa aliwatoa wana wa Israel Misri lakini hakuingia nchi ya ahadi, hakuonja maziwa wala asali kwa sababu ya tabia yake ya hasira. Wayahudi walikuwa wakimlalamikia Musa wakiwa wanahitaji maji, Musa akamgeukia Mungu na kumlalamikia; Mungu akamwambia Musa uambie mwamba huu unataka maji, lakini Musa akakasirika akapiga mwamba, mwamba ulitoa maji kwa sababu Mungu alimuheshimu Musa, lakini hasira ilimponza Musa na kumsababisha kuishia jangwani. Mwanangu fanya mabadiliko ya tabia zako ili uweze kumiliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*