Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

NENO LA SIKU.

Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 20/01/2024.
Kama unataka Rehema za Mungu zikae na wewe kwa sababu ya uovu wa baba na mama zako na unataka uondokane na hayo soma kitabu cha Wakolosai, Efeso, Mathayo, Nehemia na Ezekiel. Hivi vitabu vipo ili kuonyesha Rehema za Mungu kwetu, unaposoma vitabu hivi utaona Rehema za Mungu katika maisha yako.
Lakini kama unataka kuona Utukufu wa Mungu ukifunika maisha yako soma vitabu vya Samweli, Wafalme, Waamuzi na Ufunuo, utajiona ukiwa umefunikwa na Utukufu wa Mungu.
Jifunze namna ya kukamata mambo ya Mungu usisome tu Biblia kama hadithi soma huku ukijua unahitaji nini na kinapatikana wapi.
Mathayo 7:7-8 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”
Kama unataka kufanya miujiza, Matendo Makuu ya Mungu yakadhihirike kwako na Upako utiririke juu yako, soma kitabu cha Mambo ya Walawi, Petro, Zaburi, na Wakorintho, hapo utapata Vipawa na Karama za Roho Mtakatifu nawe utajua jinsi gani ya kudhihirisha Nguvu za Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*