Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

AMUA KUUA MWILI ILI UWEZE KUTEMBEA NA MUNGU.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe: 12.02.2024
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawashi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.”
Unautoaje mwili wako kuwa dhabihu iliyo hai?
• Ufundishe mwili wako kwa kufunga.
Usifunge kwasababu umeambiwa ufunge, bali ifanye iwe desturi yako.
Daniel 1:15 “Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.”
Mwili ukishatiishwa, Mungu anaruhusu nafsi yako ipate nguvu kutoka juu.
1. Jitenge na wanadamu wenye maneno mengi na punguza kuongea. Ruhusu nafsi yako kuongea na Mungu peke yake.
2. Punguza safari yaani mizunguko isiyo na sababu.
3. Jifunze kusamehe wanadamu wanaokukosea.
4. Pata muda wa kuchambua Biblia na usome vitabu vya watu waliofanikiwa kupitia hiyo njia.
Sasa ukishafikia hatua hiyo Mungu anafanya marejesho kwako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*