Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

MAHUBIRI JUMAPILI TAREHE 10/03/2024

Watch Now

Download

MAHUBIRI JUMAPILI TAREHE 10/03/2024

Kila jambo kuna mahali linaanzia na kuishia, kuna kipindi cha kuanza na kipindi cha kumaliza, na mwanadamu anakipindi anazaliwa na kuna kipindi ana kufa.
Wewe unapaswa kutambua kuwa upo safarini, kuishi ni safari hata kama unazunguka unaenda mahali na kurejea tena nyumbani lakini unapaswa kutambua kuwa upo safarini.
Warumi 1:28 “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.”
Kwa sababu walikuwa katika tamanio la kumkataa Mungu ndipo Mungu aliwapa kile walichokitamani na akawaacha wafuate akili zao zisizofaa. Akili isiyofaa itakupelekea ufanye vitu visivyofaa, yaani kufanya vitu bure visivyo na faida, hakuna uimara wala muendelezo huko ndiko kufanya vitu visivyofaa.
Ukiendelea kutokumtafuta Mungu utaishia kufanya vitu visivyofaa na hii itakufanya ulie baadae. Ukimuacha Mungu akilini mwako itakusababisha ulie mwishoni, ukiona watu wakitafuta msaada, wako chini ya mateso na maumivu fahamu kwamba hapo mwanzo walimkataa Mungu katika akili au fahamu zao.
Tangu mwanzo wa uumbaji Mungu aliweka kila kitu kwa utaratibu Mungu aliufanya ulimwengu wote katika mpangilio, aliweka jua litoke mashariki kwenda magharibi, ni mtu mmoja tu alifanikiwa kubadilisha hilo ambaye ni Yoshua na ni kwa sababu alimtii Mungu, aliweza kusimamisha jua.
Ili mbegu izae matunda ni lazima uizike ardhini na ife ndipo iweze kuota, vivyo hivyo Mungu alimfanya mtu kama alivyotaka, ndio maana unaweza kuona wewe ni mfupi lakini mwanao akawa mrefu ni Mungu ndiye ametaka.
Kazi kubwa ni kupata ufahamu na ufahamu ni akili ya Mungu hivyo ukiwa na ufahamu basi unayo akili ya Mungu, ukipata ufahamu lolote utendalo uko pamoja naye kwa sababu una akili yake na lolote ufanyalo analithibitisha.
Unapataje ufahamu? Pale unaporuhusu akili yako itenganishe kipi kilicho bora kwa Mungu na kipi kilichobora kwako na kipi kilichobora kwa wanadamu, na pia kuiruhusu akili yako ibainishe ni kipi kibaya kwa Mungu, kipi kibaya kwako na kipi kibaya kwa watu, ukishaweza kubainisha kwa namna hiyo ndipo sasa unaweza kusema sasa nimeanza njia ya ufahamu.
Ukiwa katika njia ya ufahamu ndiyotunaiita njia ya Mungu, anasema “njia zangu sio njia zenu na njia zenu sio njia zangu” lakini ukiwa na ufahamu basi unatembea katika njia yake kwa maana hauwezi kutembea katika ufahamu kama haupiti katika njia zake na mara zote yule anayetembea katika njia zake anakuwa tofauti na wengine.
Mwanzo 1:1-3 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.”
Ilikuwa ukiwa na utupu kwa sababu mtu hakuwepo katika nafasi yake, Mungu alijua kuwa anamuhitaji mtu awepo pale na kufuata maelekezo yake ili kuifanya dunia iwe bora kama ilivyo.
Kazi kubwa tuliyonayo sisi wanadamu huku duniani sio kulima, kujenga majengo, kufanya kazi maofisini au kwenye makampuni, la! Bali kazi kubwa tuliyonayo ni kupata ufahamu kwa maana pasipo ufahamu hakuna utakalofanya. Leo hii kuna maskini na wahitaji wengi, uchache mwingi kwa sababu ni wachache mno wanaufahamu. Kwa sababu ya wale wachache wanaojua wanaisababisha dunia iwe kama ilivyo, kama ingekuwa ni asilimia kumi (10%) ya watu wenye ufahamu dunia hii ingekuwa ni kitu kingine, lakini kwa bahati mbaya ni asilimia tatu (3 %)pekee ya watu wenye ufahamu na asilimia kumi (10%) wanawafuata wale asilimia tatu (3% ) ya wenye ufahamu na kusababisha dunia iwe kama ilivyo. Lakini hawa asilimia tatu (3% ) wanaishi kama wafalme wakiwaelekeza hawa asilimia kumi (10%) kufanya kazi ili waweze kuifanya dunia iwe kama ilivyo lakini asilia themanini a saba (87%) ni walaji hawazalishi chochote, je! Wewe uko wapi.
Kuanzia leo matamanio ya moyo wako yatatimia na hakuna kitakachozuia hayo matamanio yasitimie kwa sababu matamanio yako yana kusudi la Bwana nawe ni wa Bwana na palipo na Bwana hakuna kushindwa, kwa hiyo matamanio uliyonayo ni ya Bwana na yatatimia.
Lije litakalokuja na lenyewe litapita kama mengine yalivyokwisha kupita lakini lile la Bwana lililo sawa sawa na matamanio ya moyo wako litatimia na kuthibitika kwa sabab ohu ni la Bwana.
Usiende na matukio, wana wa Israeli waliishia jangwani kwa sababu ya kusikiliza matukio ya wale wapelelezi 10 waliorudi katika nchi ya ahadi na kusema waliona majitu marefu yanayokula watu hivyo na wao wakaingiwa na hofu. Iko hivi, ni kweli wewe ni mdogo kuliko matatizo yanayokusumbua, lakini aliye na wewe ni mkubwa kuliko yale yanayokusumbua au yule anayekuja kinyume chako; Je! Wewe unaelewa nini? Ondoa macho yako kweye yale unayoyaona ni makubwa sana kwako na ukaona kuwa yatakushinda. Hayo yanayokuja yangekuwa na nguvu yangekwisha kukumaliza, kama hayajakumaliza inamaana kuwa hayana uwezo hivyo toa macho yako huko.
Mwanangu yaache hayo yanayokuja yapite, Huu ni mwaka wako wa kuona na kupokea yale yaliyo ya Bwana, Mungu akafungue macho yako ili upate kuyaona.