Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO: UFAHAMU 1

NENO LA SIKU.
Na Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Tarehe: 11/3/2024.
Mithali 8:10-11 “Pokea mafundisho yangu, wala si fedha, Na maarifa kuliko dhahabu safi. Maana hekima ni bora kuliko marijani; Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.”
Maarifa na Hekima vina thamani mno kuliko hicho unachokitafuta, kwa sababu ukiwa na Ufahamu na Hekima una zaidi ya fedha, na ukiwa na huo Ufahamu na Hekima unaishia kuwa tajiri kwa maana Hekima itakuongoza kupata kila unachokihitaji katika maisha yako.
Mithali 8:18-21” Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia. Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi, Na faida yangu hupita fedha iliyo teule. Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao.”
Utajiri sio vitu bali ni jinsi ulivyo, kwa maana hiyo kwa namna ulivyo inaweza kukufanya wewe uwe tajiri na mtu aliye stawi lakini pia kwa jinsi ulivyo inaweza kusababisha uwe maskini, kwa maana utajiri au umaskini unatoka ndani yako na sio nje. Ki vipi? Kwa namna unavyowaza na namna unavyotamka, nini unatoa wewe ndani yako kwa maana chochote utakachokiwaza ndicho utakachokisema na ndicho kitakachokuwa katika maisha yako.
Mwana wa Mungu ukitaka kufanikiwa katika maisha yako badili namna unavyowaza na unavyotamka. Sema unavyotaka kuwa sawa sawa na ulivyosikia na ndivyo itakavyokuwa kwako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*