Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO: UFAHAMU 2

NENO LA SIKU.
Na Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.
Tarehe: 12/3/2024.
Mithali 8:20-21 “Natembea katika njia ya haki, Katikati ya mapito ya hukumu. Niwarithishe mali wale wanipendao, Tena nipate kuzijaza hazina zao ” Yeyote mwenye Ufahamu anatembea katika haki na kwa sababu hiyo Mungu anaanza kumhukumu kwa haki. Faida ya kuwa mwenye haki ni ipi? Mungu anakuwa Mpaji wako na anakuhumia utajiri.
Ufahamu ni kujua kipi ni kizuri kwa Mungu, kipi ni kizuri kwako na kipi ni kizuri kwa watu, kipi ni kibaya kwa Mungu, kipi kibaya kwako na kipi ni kipaya kwa watu.
Jihukumu mwenyewe usisubiri watu wakuhukumu, acha akili yako ikuhukumu na sio kuhukumu watu. Watu wengi wanapenda kuhukumu watu na sio kujihukumu wao wenyewe na ndio maana wanaishia kuwa maskini lakini ukijua kujihukumu mwenyewe katika yale unayoyatenda basi utabadilika, lakini ukihukumu wengine hautakaa ubadilike bali utawachukia wale wanaotaka ubadilike na wewe hautaishia popote.
Yeyote anayetembea katika hiyo njia ya haki ni yule anayempenda Mungu kwa maana hauwezi kutembea na mtu usiyempenda; upo na mume wako kwa sababu unampenda na kwa sababu hiyo mnafanya kila kitu pamoja, ukimpenda Mungu utatembea katika njia zake na utatii maagizo yake, njia zipi hizo? Haki yake, Mungu akiliona hilo pendo ndani yako ndipo sasa Yeye atakuja na kukubariki.
Katika kupata Ufahamu kuna ugumu; Musa alichukua miaka 80 ili kupata Ufahamu lakini Daudi alichukua miaka 15, Yeremia kwa miaka 12 akapata Ufahamu, mimi sijui kuhusu wewe itakuchukua miaka mingapi, mimi nilipofikisha miaka 30 nikapata Ufahamu. Muombe Mungu akupe Ufahamu na Hekima kwa maana ukipata Ufahamu umepata kila unachokihitaji katika maisha yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*