Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO: UFAHAMU 3

NENO LA SIKU
Na Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
Tarehe: 13/3/2024
Isaya 65:24 “Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.”
Ukiwa na ufahamu wa Mungu utakupa kuomba sawa sawa machoni pa Mungu na utakapoomba sawa sawa na ufahamu utamfanya Mungu ajibu kabla haujaomba kwa maana ufahamu ni akili ya Mungu hivyo Mungu hawezi kuinyima akili yake bali ataitimiliza kwa maana katika akili ya Mungu ndipo palipo na ufahamu wake.
Kupitia ufahamu waliokuwa nao Yoshua na Kaleb ulisababisha Mungu awalinde pale watu walipotaka kuwapiga mawe mpaka kufa, baada ya waliposema kile walichokiona na kukiamini kuhusu nchi ya Kaanani. Sawa sawa na walivyosema Mungu aliwapa kuimiliki nchi ya Kaanani, wengine walikufa jangwani lakini hawa wawili kwa sababu ya ule ufahamu wa Mungu waliokuwa nao Mungu aliwatunza mpaka mwisho ili waweze kumiliki kile walichosema na kukiamini.
Unaponena sawa sawa na ufahamu Mungu atakupa kile ulichosema. Mungu hawezi kumtumia mtu ambaye hana ufahamu (imani), Lakini ukiwa na ufahamu atakusababisha ukipate kile unachotamani na zaidi ya hicho ulichokitamani.
Mara zote sema unachotaka kukiona sawa na unachotaka kukisikia. Unapotamka unachotaka kitokee ndicho utakachopokea. Usiangalie mazingira yatakusimamisha, bali wewe tamka unachotaka kitokee huku ukiamini kuwa kitakuwa kwako pasipokuwa na mashaka na Mungu akiona imani yako atakupa kile unachokitaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*