Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

SOMO: UFAHAMU 4

NENO LA SIKU
Na Mtume Na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
Tarehe: 14/3/2024
1 Yohana 5:14-15 “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”
Unapokwenda mbele za Mungu kuomba akilini mwako unawaza nini? Je! Unajua ya kuwa hayo maombi yako Mungu atayajibu, au unaomba kwa sababu ni wajibu wako kuomba? Biblia inasema “na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.” Ukijua kuwa Mungu akusikia basi utakuwa na imani ya kuwa Yeye atakupa kile ulichokiomba.
Kwa nini umeomba sana lakini haujapokea kile ulichokiomba? Ni kwa sababu ya mashaka uliyokuwanayo ndani yako. Kabla haujaomba fahamu unaenda kuomba nini, Kabla haujatenda au kusema chochote kwanza pata ufahamu juu ya hilo jambo ili utakapokwenda kulifanya au kuomba uweze kulipokea.
Unaelewa nini kabla ya kutenda jambo? Kile unachokielewa ndicho kitakachokupa kupokea sawa sawa na ulichokielewa. Watu wanafanya vitu pasipo kuelewa, unakuta mtu anafungua duka kwa sababu amemuona fulani amefungua duka na anapata wateja wengi, au anaanzisha biashara kwa sababu hana kitu cha kufanya, la! Ni bora usifanye kwa sababu hautapata chochote, pata ufahamu kwanza wa kile unachokwenda kukifanya kabla ya kutenda, na huo ufahamu utakupa wewe kutambua kile unachoenda kukifanya na namna ya kukifanya ili kiweze kuzaa matunda kwako na sio hasara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*