Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 14/04/2014

Watch Now

Download

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 14/04/2014

SOMO: IBADA
Tunapo zungumza kuhusu ibada maana yake tunazungumza moyo wa mtu na Mungu na sio mioyo ya kundi la watu.
Mithali 8:30-31 “ Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; Nikawa furaha yake kila siku; Nikifurahi daima mbele zake; Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu; Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.”
Kuna kitu ambacho Yesu alikifurahia kwa ajili ya Mungu, furaha aliyokuwa nayo Yesu ilikuwa ni kukaa pamoja na Baba yake, kazi yoyote aliyokuwa akiifanya ilikuwa ni ili kumfurahisha Baba yake. Leo hii kuna watu wapo kanisani na wanasema wanamtumikia Mungu lakini wanauchungu na hasira mioyoni mwao. Yesu Yeye anasema alifanya kazi na akawa furaha kwa Baba yake wa Mbinguni, kama Yesu furaha yake ilikuwa pamoja na wanadamu maana yake aliona ramani ambayo Mungu alikuwa nayo juu ya wanadamu, hivyo Yesu akasema furaha yake itakuwa na mtu yeyote atakayempenda Baba yake.
Kabla haujazaliwa Yesu alifahamu sura yako ya kwamba itatokea duniani hivyo Yesu akawa akifurahia kuwa watakuwepo wanadamu wenye kumfurahia Mungu kama alivyo Yeye, je wewe ni mmoja wao wa wale wanaomfurahia Mungu au la?
Kutoka 20:1-3 “ Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.”
Hapa Mungu alikuwa akimwambia Musa kuwa aongee na wana wa Israel, alitaka awawekee utaratibu wa ibada na amri za kuzifuata, alikuwa akiwaambia wana wa Israel wakumbuke kule walikotoka na watambue kuwa sio kwa ujanja wao bali Mungu alitumia uwezo wake kuwatoa Misri.
Mungu aliweka agizo kwa wana wa Israel na kusema “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” maana yake ni kuwa Mungu alitamani kusifiwa Yeye pekeyake na ukimsifu Yeye anafurahi. Unapoweza kumsifu Mungu ndipo mbingu zinafunguka na Mungu akiona hilo ndipo mapigo yake anayageuzia kwa ibilisi na wewe unakuwa salama.
Matokeo ya kuabudu miungu mingine ni yapi? Kutoka 20:5 “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,”
Huu ndio wivu wa Mungu kwa wale wanaoabudu miungu mingine, wale wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji, wanaofanya ibada za sanamu wanaofanya matambiko. Wewe unayemjua Mungu amua kumwabudu Yeye pekeyake wala usimchanganye Mungu na vitu vingine kwa maana Mungu anasema “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”
IBADA INAAMBATANA NA VITU VIFUATAVYO:
1. Utii:
Kama hakuna utii hakuna ibada, utii unahusika hata na kile kitu usichokipenda ilimradi umeamriwa kukifanya.
2. Heshima:
Ibada inaambatana na heshima, unapomuheshimu Mungu katika kuabudu unajaliwa kupewa hazina zilizofichwa. Kutoka 20:12 “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.”
Tukimuheshimu Mungu na akitambua kuwa tunampenda na tukisikia sauti yake tunatii na kufanya, ndipo Yeye atatufungulia hazina zilizojificha.
3. Unyenyekevu;
1 Petro 5:6-7 “ Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” Mtu yeyote aliye mnyenyekevu anakubaliwa na watu na Mungu huwa anamkweza.
4. Shukrani:
Luka 17:11-19 “……….. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.”
Mungu anafurahishwa sana na watu wenye shukrani, ukimshukuru Yeye anaweza kufanya zaidi ya vile ulivyoomba.
5. Utukufu:
Mungu hapendi kugawana utukufu na mwanadamu, mtu akikutendea kitu jua kuwa ni Mungu dio amemtumia huyo na kukupa wewe hivyo utukufu unapaswa kumrudishia Mungu.
• Isaya 42:8 “Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.” Isaya 4811 “Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.”