Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

IBADA JUMAPILI TAREHE 14/07/2024

Watch Now

Download

IBADA JUMAPILI TAREHE 14/07/2024

SOMO: SAFARI YA UMILIKI
Mwanzo 12:1-3 “BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.”
Kuna baadhi ya watu Mungu aliwainua ndani ya Biblia ambao wakitaka jambo fulani linalohusiana na kule wanapokwenda, Mungu aliwapa neema ya ubaba ya kufungua lango hilo, kati ya watu hao ni Ibrahimu baba yetu wa Imani; alifungua lango hilo la Imani.
Kwa nini Ibrahim alifanyika nguzo na mlango kwetu?
Isaya 51:1-2 “……… Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.”
Isaya anatukumbusha kuwa inapokuja swala la kupokea ahadi na umiliki tunapaswa kumuangalia Ibrahimu aliye baba yetu wa Imani. Neno linasema wote walio wa Kristo asili yake ni Ibrahimu, kwa nini tumuangalie?
Yako mambo ambayo kila Mkristo aliyeitwa anapaswa kuyatambua:
1. Wito wa kutoka: Wito huu ndiyo unaokufanya wewe uokoke, wito huu ni wakipekee sana kwa maana kabla ya Yeye kukuita Roho wake alikuwa anafanya kazi ndani yako kwanza alianza kufanya maandalizi ya kukuchagua. Lakini inapokuja majira na nyakati ndipo unaitika na kufanywa kuwa mwana.
Unaweza ukawa na mchecheto wa kutumika lakini kabla ya majira na nyakati kufika hautaweza kufanikiwa.
Wakati Mungu anamwambia Ibrahimu atoke, kuna mambo mawili ambayo Mungu aliweka ndani yake:-
• Urithi
• Uzao
Pamoja na kwamba Mungu alimuahidi urithi lakini pia alimuahidi kumpa uzao, na kwa kupitia uzao atafanyika kuwa kuhani kwa mataifa.
Mungu aliposema tumuangalie Ibrahimu alikuwa anataka tuangalie asili ya wito wake, majukumu, matarajio na ahadi ya wito wake. Kila mmoja aliyeitwa (aliyeokoka) kuna hatua ya kufanyika kuwa Taifa;1 Petro 2:9 “ Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;”. Wewe umeteuliwa kama vile Ibrahimu alivyo teuliwa, wewe uliyekuja kwa Kristo safari yako ilianza baada ya kuteuliwa. Ndani ya wito tulioitiwa kuna kazi tuliyopewa ili kuupatanisha ulimwengu na Mungu, wewe ni Taifa Takatifu.
Yohana 6:44 “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.” Hakuna anayeweza kwenda kwa Mungu isipokuwa amepelekwa, wewe uliyeokoka unapaswa kumshukuru Mungu maana umechaguliwa.
Yohana 15:16 “Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.” Wewe uliyeokoka haujajichagua bali umechaguliwa.
Katika wito wa wokovu, jambo la kwanza tunaloliona ni Urejesho wa mahusiano. Unaweza ukawa umeingia katika huu wito (umeokoka) lakini bado tabia zisizoendana na uwana zinakuandama, hiyo ni hatua ya uchanga unafanya maandalizi ya kuingia kuwa mwana, na hatua hiyo ya uchanga siyo hatua ya umiliki.
Waefeso 1:13-14 ”Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.”
Kilichopotea wakati wa Adam ilikuwa ni umiliki, lakini ili umiliki urejee kwako kitu cha kwanza ni kusikiliza neno ambalo hilo neno litakufanya ugongwe muhuri ambao utakuingiza katika umiliki wako (wokovu).
Mungu siyo tu aliahidi ukombozi bali alilipa malipo yote kwa udhihirisho wa Roho wake, wewe uliyeokoka umegongwa muhuri wa Roho, huo muhuri ni uthibitisho kamili ya kwamba unastahili umiliki wote wa ulimwenguni na kisha uzima wa milele, kwa maana siku ya mwisho utaangaliwa huo muhuri na kukuhakikisha kuwa wewe ni mwana wa Mungu.
KRISTO KUZALIWA NDANI YAKO:
Hatua ya Kristo kuzaliwa ndani yako ndiyo hatua ambayo itakutoa katika utoto na kufanyika kuwa mwana mahali ambapo utamiliki.
Wewe uliyepokea wito kwa kusikia neno la Mungu na hata kupokea wokovu, umefanyikaje kuwa mwana wa Mungu? Yohana 1:12 “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;”
Mbegu ya uwana huwa haishindwi, wewe ulieyokoka haushindwi na chochote, kama walivyompeleka Yesu msalabani wakafikiri kuwa wamemaliza, lakini hawakujua kuwa ndiyo walikuwa wanatangaza tangazo la Ushindi kwake.
Mwana wa Mungu wewe uliyeokoka hali yoyote ambayo unapitia na kuona kuwa hauwezi utaishinda, maadamu tu umeishikilia ile ahadi ya uwana, usiangalie mazingira bali muangalie yule aliyekufanya kuwa mwana naye atakushindia.
MAOMBI:
1. Bwana Yesu nimekubali kufanyika kuwa mwana ninayeaminiwa na Baba yangu wa Mbinguni.
2. Huu ni mwaka wa kumiliki kwangu Bwana nipe kumiliki sitaki kuwa wa kawaida.
3. Bwana teketeza kila pando ndani yangu linalonifanya nisiuendee umiliki wangu.
TANGAZA:
Leo natangaza kuwa mimi ni uzao uliyobarikiwa, ni kuhani wa kifalme mtu wa milki ya Mungu, nitaingia kunako umiliki wangu na kamwe hakuna kitakachonizuilia na wala hatachukua mtu mwingine.
© Katibu Mkuu wa Kanisa la Efatha- Prof. Emmanuel Chao