Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

TABIA YA KUNUNG’UNIKA NA KUDHARAU.

NENO LA SIKU.
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha.
TAREHE 22/07/2024.
Kutoka 14:11 “Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?”
Wana wa Israeli walikuwa na tabia ya kunung’unika kila wanapopata kikwazo kidogo, badala ya kutulia na kufikiri vizuri. Watu wengi hata sasa wanaona Mungu akitenda Mambo Makuu mbele ya macho yao, utawaona wakishangilia kwa vigelegele na makofi. Baada ya kitambo kidogo, kikwazo kikitokea wanasahau na wakati mwingine wanatoa maneno magumu kwa wapakwa mafuta wa Bwana.
Hali ya kunung’unika ikimvaa mtu, itamtesa sana na ikiumbika ndani yake, itamletea madhara makubwa sana. Tabia ya kunung’unika haiwezi kuruhusu msamaha na mara zote mnung’unikaji yeyote kusamehe kwake kuna kuwa ni ngumu sana.
Biblia inatuambia kuwa watu wa aina hiyo wataadhibiwa; Yuda 1:15-16 “ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake. Watu hawa ni wenye kunung’unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.”
Mwana wa Mungu Baraka za Mungu huambatana na tabia aliyonayo mtu, hivyo kama unataka kufanikiwa kupokea Baraka zake katika maisha yako ya sasa na yale yajayo, kuwa mwangalifu sana na tabia yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*