Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

AMUA KUKAA NDANI YA KRISTO.

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 11/1/2024.
2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”
Tunamshinda ibilisi baada ya kuelewa kile Yesu alifanya pale Msalabani, ukishaelewa jambo hilo basi utakuwa na Ushindi wote.
Kama mtu yeyote akiwa ndani ya Kristo, Neno linasema AKIWA NDANI sio pamoja wala karibu bali AKIWA NDANI YA KRISTO, mtu akiwa pamoja na kitu ni rahisi kutengana na hicho kitu kuliko kikiwa ndani yake, kwa maana ukitaka kukichukua kitu kilicho ndani ya mtu lazima umuue ndipo uchukue, lakini kilicho pamoja nawe ni rahisi kukichukua
Tumezaliwa mara ya pili pale tulipokubali kufa ndani na tukaruhusu kitu kipya kiinuke ndani yetu.
Je! Wewe uko ndani ya Kristo?
Mtu anaposema Yeye ni kiumbe kipya anamaanisha nini? Anamaanisha hauwezi kwenda ndani ya Kristo kama ni mtu yule yule, unapoingia ndani ya Kristo ndipo unakuwa mpya.
Umezaliwa kwa mwili pale ulipotoka katika tumbo la mama yako, lakini ili uzaliwe mara ya pili ni lazima uingie ndani na sio utoke nje.
Umezaliwa ki mwili kwa kutoka lakini ili uwe Mtakatifu ni lazima uingie Ndani. Usibaki nje bali ingia Ndani sio kwa mama yako bali kwa Yesu Kristo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*