USHUHUDA
Naitwa Optatus Octavian, nilikuwa na mgogoro baada ya kununua shamba lenye ekari sabini (70) na shamba hilo likauzwa kwa watu wawili tofauti na ndipo uongozi wa kijiji ulipoamua tugawane nakuamua mimi nipewe ekari 40. Namshukuru Mungu baada ya kuchangia fedha kwa ajili ya Kusanyiko hili nimepigiwa simu na kuongezwa ekari kumi na saba (17) na kufika jumla ya ekari hamsini na saba (57) na nimekabidhiwa na muhtasari bila hata kikao.