Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Baada ya kuokoka Mungu ametusaidia mimi na mdogo wangu tumerudi shule.

Naitwa Peter Christopher napenda kumshukuru sana Mungu kwa matendo yake makuu katika maisha yangu na kwa familia yangu pia, baada ya baba yangu kufariki nilikosa tumaini tena la kuishi kwa maana yeye ndiye tuliyekuwa tunamtegemea, kwa maana kipindi hicho nilikuwa chuo na nikaishia kufeli. Baada ya baba yangu kufariki niliamua kuja Dar es salaam nikitokea Musoma nikiwa na lengo la kuja kufanya kazi ya kuosha magari, nilipofika huku Dar nilikosa sehemu ya kufikia kwa maana nilipokuwa nategemea walikataa kunipokea.
Nilihangaika kwa kipindi, ilifika mahali nilikata tamaa kabisa ndipo nikakutana na mtu mmoja anayesali Efatha, akanishuhudia habari za Yesu nikaamua ni bora tu niokoke. Baada ya mimi kuokoka ndipo maisha yangu yakaanza kubadilika, katika kusanyiko kuu la mwaka jana nilitoa ahadi ya kitabu shilingi laki moja na sikujua pesa naitoa wapi, na mwaka huu baada ya kusanyiko nikaahidi pesa nyingine ya ujenzi shilingi laki moja pia sikujua naitoa wapi. Baada ya ibada ya jumapili nikawa namuomba Mungu anisaidie niweze kuzikamilisha ahadi zote nilizozitoa. Nikiwa njiani narudi nyumbani nilipigiwa simu na kaka yangu anayeishi Marekani akanitumia namba ya simu nimtafute huyo mtu yupo huku Dar es salaam nilipomtafuta akaniambia niende mahali alipo, nikiangalia mfukoni nimebakiwa na shilingi miatano tu nayo ni nauli ya kunifikisha hapo huyo mtu alipo nikamwambia Bwana Yesu mimi sijui itakavyokuwa ila najua wewe upo pamoja na mimi. Nilipofika kumbe kaka yangu alikuwa amenitumia fedha nyingi tu, nilimshangaa sana Mungu, baada ya kuichukua ile fedha nikalipa madeni niliyokuwa ninadaiwa na fedha iliyobaki nikaenda kulipa ada ya chuo na sasa nipo Chuo mwaka wa pili katika chuo cha Afya Lugalo, lakini pia ndugu yetu mwingine akasema atamlipia mdogo wangu ada ya chuo na yeye amekuja Dar es salaam amejiunga na chuo cha IFM.
Hakika Mungu anaweza, mimi niliyekuja kama muosha magari baada ya kukutana na huyu Yesu amebadilisha maisha yangu na kunirejeshea elimu yangu ambayo nilidhulumiwa, hakika kwa Mungu hakuna linaloshindikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*