Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Namshukuru Mungu Nimesaini mkataba wa kazi na kampuni kutoka Kenya.

USHUHUDA
Naitwa Phidesia Mwakitalima, namshukuru Mungu sana siku ya Jumatano tarehe nne mwezi huu wa kumi, Katika Kusanyiko Kuu la Efatha linalofanyika kila mwaka Precious Centre Kibaha, tulitamkiwa baraka nyingi sana na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, moja ya baraka alizotamka alisema “ kuna watu wanaenda kuwa na fedha nyingi watatembea na wahasibu wao wakiwasaidia kuhesabu fedha na kutengeneza matumizi”.
Baada ya kutoka kwenye Kusanyiko nilipofika nyumbani usiku wa manane nikiwa nimelala nikasikia sauti ya Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira anaamrisha watu anawaambia wanipe fedha kiasi cha shilingi milioni 100 lakini kuna sauti za watu wakawa wanalalamika kwa nini nipewe mimi na nina fedha nyingi, kwa nini wasipewe wengine, nilipoamka nikatengeneza maombi nikamwambia Mungu lazima nipate hizo fedha nilizosikia.
Namshukuru Mungu wiki iliyopita nilipigiwa simu na kampuni moja toka nchini Kenya wakitaka niwasaidie kufanya kazi zao hapa Tanzania katika mikoa minne, Mkoa wa Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya, wakanishindanisha na kampuni nyingine na sikuwa nawafahamu lakini kwa neema ya Mungu nilifanikiwa kupata ile kazi, tukakubaliana kusaini mkataba wa mwaka mmoja na kazi hiyo ilihitaji niwe na mhasibu, mtu wa masoko na wafanyakazi watano kutoka katika mikoa hiyo. Namshukuru Mungu wafanyakazi wote wameshaanza kazi, nimemshangaa sana Mungu kwa kulidhibitisha neno la Mtumishi wake Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira kwa muda mfupi sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*