Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Dhambi ndio chanzo cha matatizo

NENO LA SIKU.
Tarehe: 15/11/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Yohana 16:8-11“Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.”
Dhambi ndio chanzo cha magonjwa, maradhi, umasikini na kupambana kwako, ikiwa utaamua kuondoka katika maisha ya dhambi na kuishi maisha ya haki, magonjwa, maradhi na umasikini havitakuwa na nafasi kwako.
Ukisoma Biblia utaona kuwa Mungu hajawahi kumuacha mwenye haki wake akakosa chakula, kwa nini kwako wewe uliyeokoka unateseka na kung’ang’ana? Kwa sababu haujaamua kuacha dhambi.
Unaweza kujiuliza kwa nini watu wengine hawajaokoka na wanaishi maisha ya dhambi lakini wanaendesha magari na wanaishi maisha mazuri? Ndio wameacha kumpenda Mungu na wakaukimbilia uovu, wako kwenye uovu na Biblia inasema usiwaonee wivu wao, wako hivyo walivyo ili kwamba waangamizwe milele, lakini kwako wewe ambaye umeamua kumpenda Mungu ipende haki, kwa wewe kufanya hivyo kamwe hautapungukiwa na chochote unachokihitaji katika maisha yako na unapohitaji usaidizi kwa Mungu wakati wowote utaupata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*