Haki ya Mungu kwako

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 15/10/2024.
Kila mtu huku duniani ana ratiba yake ambayo Mungu amempangia na ili uweze kuvipata vile Mungu alivyokuandalia ni lazima utembee katika kweli ya Mungu ili uweze kuipata haki yako.
Mara zote usipende kumuomba Mungu akupe kufanana na mtu fulani? La, kwa sababu unapoomba Mungu akupe kuwa kama mtu fulani ina maana kuwa utapata ambacho sio chako. Mfano; haki ya Daudi ilikuwa afikie kuwa mfalme katika njia aliyopitia yeye; lakini haki ya Yusufu ilikuwa lazima akawe mtumwa katika nyumba ya Potifa, aende jela ndipo akawe mkuu katika ufalme, sasa unapoomba wewe kuwa kama mtu fulani ina maana utapewa kitu ambacho sio cha kwako na itakuwa ni ngumu wewe kushinda. Lakini ukiomba sawa sawa na haki yako hata likitokea gumu la aina gani hautakata tamaa bali utasonga mbele.
Utajuaje upo katika njia sahihi? Lolote linalotokea mbele yako hata kama ni gumu kiasi gani haukati tamaa na unapata nguvu ya kuendelea mbele.
Unapoomba Mungu nipe kupita katika njia yako sawa sawa na haki yako kwangu, Yeye anakupa nguvu ya kushinda yale yote yanayokuja mbele yako. Usiombe kuwa kama Daniel kwa maana je! Ukiingizwa katika tundu la simba utaweza? Wewe paka tu unaogopa sasa ukiingizwa katika simba utabaki kweli?
Ombi lako kwa Mungu liwe ni;
Omba Mungu akupe kuwa sawa sawa na haki yako aliyokuandalia ili uweze kuona baraka zake kwako.

Add Comment