Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Imani

NENO LA SIKU
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
Tarehe 18/12/2023
Yoshua 1:3 “Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.” Hii inamaana kuwa chochote utakacho fanya wewe ni Mshindi na umepewa kumiliki.
Imani ni mtaji wako, kama unaamini popote utakapo kwenda kuchukua hatua au lolote utakalo kwenda kulianza litatimizwa ondoa mashaka, huu ni muda wako wa kuchukua nafasi yako.
Unapochukua nafasi yako na kuanza jambo fulani, unapokuwa katika huo Mtembeo vikwazo vipo, ukosefu wa pesa au mazingira yako yanaweza kuwa ni adui yako namba moja, lakini unatakiwa kujua kuwa Bwana amesema kuwa “Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako;” Si katika Utumishi wako tu bali hata katika maisha yako ya kila siku.
Kwa nini waamini wengi leo hii ni maskini? Ni kwa sababu ni kweli wanaamini Neno la Mungu lakini wana mashaka, Neno linasema “Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yako nimekupa” wakati huo huo unapokwenda kazini kwako unawaza wewe hauna elimu ya kutosha hivyo hauwezi kupandishwa cheo, au unapofika Kwenye biashara yako unawaza biashara yangu haina wateja hivyo naenda kufunga.
Usiruhusu vitisho vya aina yeyote ile viharibu imani yako, usiruhusu mashaka yakuweke mbali na kile unachokitarajia; kwa maana hayo ndiyo adui yako namba moja, usiruhusu sauti yoyote ya adui ikutishie chukua nafasi yako na usonge mbele, amini hata kama unaona njia ya kufanikisha hicho unachokitaka ni ngumu kiasi gani amini kuwa utafanikiwa na usiwe na mashaka hakika kitakuwa chako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*