Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Je! Unafanana na Mungu?

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 17/10/2023.
Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Kuna vitu viwili hapa, MFANO na SURA, Mfano maana yake ni Mfanano na Sura ina maana kulingana yaani kufanana. Tunahitaji kuwa kama YEYE (Mungu) kwa jinsi ambavyo tunaonekana, lakini pia tunahitaji kuwa na Mfanano, yaani chochote tunachokifanya lazima tufanye kama Yeye.
Yesu akasema tunafanya kila ambacho Baba (Mungu) anataka tufanye, hivyo kwa kupitia matendo yetu yataonyesha sisi ni mali ya nani. Namna unavyofanya au kutenda katika maisha yako, ndoa yako kutaonyesha wewe ni mali ya nani.
Baraka zinakuja kutoka kwa Mungu zinakwenda kwa wale wanaofanana nae na sio kwa kila mtu. Swali unalopaswa kujiuliza, Je! Wewe unafanana na Mungu? Au Je! Wewe ni Mfano wake? Kama ndivyo Baraka ni zako huhitaji kupigana ili uwe na Baraka. Hakikisha unaendelea kufanana na Mungu kwa Mfano wake na Sura yake muda wote ili usiku na mchana upate kulindwa na kuziona Baraka zake katika maisha yako.
Haufungi na kuomba ili uweze kuzipata Baraka kwa maana hata wenye dhambi wanazipata, jambo la muhimu hapa ni hili, Je! Unafanana na Mungu katika kutenda na kuenenda kwako? Kama ndivyo Baraka ni za kwako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*