Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Jua namna ya kumsogelea Mungu

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 18/11/2023.
Zaburi 51:1-19 “Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu…….”
Daudi alielewa kuwa chanzo cha matatizo yake kilikuwa ni kujitenga na uwepo wa Mungu. Ndiyo maana alimsihi Mungu amrehemu na ampe furaha ya Wokovu, Daudi aliomba maombi manne alipokuwa anataka kuiona furaha ya Bwana; alimsihi, aliomba, alifunga na alitubu mbele za Bwana, Daudi alifanya haya ili kuweza kumsihi Mungu amsikilize.
Kuna njia ambazo zitamfanya Mungu akukaribie, haijalishi wewe una dhambi kiasi gani lakini ukifuata ule utaratibu wake utamfanya Mungu akufurahie, kwa sababu Yeye anatafuta mtu ambaye atafanya sawasawa na mapenzi yake. Mungu hajasema kuwa anatafuta mtu maalum ili amtumikie, la! bali alisema kuwa anatafuta mtu ambaye anajinyenyekesha Kwake ili amtumikie.
Namna unavyojiandaa mwenyewe na kujali mambo ya Mungu, namna unavyofanya vitu vyake kwa kipaumbele ndivyo naye anakuweka mbele, mfanye Mungu awe kipaumbele chako cha kwanza ili aweze kukuweka juu; kwa namna unavyomfanya Yeye kuwa kipaumbele chako cha kwanza ndivyo utamfanya awe karibu na wewe. Ukishajua namna ya kuugusa moyo wa Mungu hauta hangaika kumuita Mungu bali Yeye atakuja kwako mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*