Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Kubali kuongozwa na Roho Mtakatifu.

NENO LA SIKU
Tarehe: 26/10/2023
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Luka 1:35 “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”
Roho Mtakatifu anapokuja kwako hukufunika na nguvu zake ili akuendeshe na sio kuendeshwa na nguvu ya dunia hii yaani nguvu ya dhambi, yeye anapokuja kwako anaisukuma mbali nguvu ya giza ndani yako.
Roho wa kweli ni Roho wa Bwana, Roho wa Bwana juu yako anakuongoza ili akufikishe kwenye kusudi la kuumbwa kwako na siku zote anakupa kuielewa kweli ili usipotee. Neno linasema utapokea nguvu akiisha kukujilia juu yako Roho Mtakatifu. Roho wa Mungu hutusaidia kutimiza wito mkuu. Roho wa Mungu hukaa juu yetu mara nyingi ili tuweze kumiliki.
Bwana Yesu ametangaza kwa watu aliowaridhia kuwa endapo watajawa na Roho Mtakatifu watakuwa sifa, Roho huyu atawapa maelekezo kila hatua ya maisha yao, watafanya maajabu kwa ule muungano wao, watakula na kunywa pamoja na Yesu Kristo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*