Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

KUMILIKI PASIPO MWISHO.

NENO LA SIKU.
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira- Kanisa la Efatha.
TAREHE 24/07/2024.
Isaya 43:19 “Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.”
Mungu ameumba kila mtu na Neema nyingi lakini tunatumia kiasi kidogo sana cha Vipawa alivyotupa Mungu akilini mwetu. Hii ni kwa sababu tabia yetu inazuia Akili zetu hivyo Neema aliyoweka Mungu ndani yetu haitumiki inavyotakiwa. Watu wameendelea kujidharau na kujiona hawawezi. Yatosha sasa, ifike mahali uelewe Neema aliyokupa Mungu na uanze Kumiliki pasipo mipaka; usijewekee sheria ya kushindwa.
Mungu ametuwekea ahadi ya kwamba anaenda kutenda jambo jipya; lakini wewe unafuta hiyo ahadi kutokana na tabia yako, lugha unayotumia na mawazo unayojiwazia ni kikwazo.
Unapoamua kufanya jambo lolote usiseme tena kuwa unajaribu. Kwa kawaida kila jaribio lina matokeo mawili; kufanikiwa au kushindwa, hivyo usifanye jambo lolote kwa “kujaribu tu”, bali fanya kwa uhakika wa Kufanikiwa.
Natangaza kwako katika Mwaka huu wa Kumiliki hakuna kuendelea tena kushindwa bali Utashinda na chochote ulichodhamiria kukifanya Mwaka huu Kitafanikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*