Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Linda wokovu wako

NENO LA SIKU.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira, Kanisa la Efatha.
Tarehe 21/11/2023.
Mathayo 24:3-12 “Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?……….”
Mathayo 24:10-13 “ Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.”
Upendo ndani ya Kristo hauhamasishwi kwa maana ni sheria ya moyoni. Huhitaji kuhamasishwa umpende mwingine kwa maana kama wewe umezaliwa na Mungu (umeokoka) na Yesu yupo ndani yako, Upendo uwe ni tabia yako na sio suala la kuamua umpende yupi na usimpende yupi kwa maana huo ni Uumbaji wa Mungu, hivyo huhitaji kuhimizwa kuwa na Upendo.
Unaweza ukawa umeokoka, ukafika Kanisani na ukakwazika kwa sababu ya yale yanayotokea, usiangalie hayo kwa maana Wokovu ni wako na Yesu ni wako. Unapokwenda Kanisani usiangalie tabia za watu wengine kwa maana wengine wanaweza wakawepo Kanisani ili kukosesha wengine ili washindwe kufika Uzima wa milele.
Hata Yesu alipokuwa huku duniani Yuda alikuwepo, hivyo hata Kanisani watakuwepo watu ambao hawatashiriki Uzima wa milele. Je! Wewe lengo lako la kwenda Kanisani ni nini? Linda sana Wokovu wako vumilia mpaka mwisho kwa maana Biblia inasema atakayevumilia hata mwisho ndiye atakayeokoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*