Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mfanye Mungu kuwa hazina yako ili akufanye kuwa hazina yake.

NENO LA SIKU.
Tarehe: 27/11/2023.
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira.
Mwanzo 22:10-13 “Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee…….”
Unapompa Mungu kile unachokipenda zaidi au kile ambacho mara zote unakitazama na kukitegemea kile cha thamani kuliko vyote, hapo ndipo unapomgusa Mungu ili Yeye afanye kwa ajili yako. Siku utakapoamua kumpa Mungu hazina yako masumbufu yako yamekoma kwa maana Mungu atakufanya wewe uwe hazina yake na kamwe hautapungukiwa.
Mungu alimjaribu Ibrahimu na akaona yupo tayari kutoa kilicho cha thamani Kwake, ndipo malaika wakamwambia “kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu”, Kuja Kanisani kila siku sio kwamba ndio unampenda sana Mungu? Kuna watu wanakuja Kanisani kwa sababu wanaogopa kuzimu; Lakini ili uonyeshe kwamba unampenda Mungu ni pale unapotoa, wewe unatoa nini kwa Baba yako wa mbinguni? Kile unachokitoa ndicho kitaonyesha kama unampenda Mungu au unaenda Kanisani ili kuikwepa kuzimu.
Unapompa Mungu kilicho bora kuliko vyote utaisababisha Baraka ya Mungu na heshima iwe kwa ajili yako milele. Jifunze kutoa kilicho bora, unapotoa kilicho bora ina maana kuwa unaachilia Baraka za Mungu kuwa na wewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*