Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mnganga wa kienyeji aokoka baada ya kuhubiriwa akiwa gerezani

USHUHUDA
Naitwa Malima Gambo, napenda kumshukuru sana Mungu kwa kuniokoa; tangu nilipokuwa mtoto mdogo nikiwa na umri wa miaka saba nilikabidhiwa mikoba ya kiganga na nikawa nafanya kazi ya uganga. Baada ya kuwa mkubwa nikaoa nikiwa Mkoani Simuyu; baada ya kitambo nikahamia Mkoa wa Pwani nikiwa na kazi yangu hiyo hiyo. Nilikuwa na watoto wangu wawili, mtoto wangu mmoja aliugua ugonjwa wa ajabu sana akawa anakojoa damu kwa kuwa nilikuwa mganga nilijua kuwa naweza kumponya.
Nilihangaiaka baada ya kuona nimeshindwa ndipo nikampeleka kwa mganga mwenzangu ambaye alikuwa na nguvu kuliko mimi, tulikubaliana kuwa akimponya mtoto wangu nitampa sehemu yangu ya ardhi. Yule mganga akamtibu lakini hakupona na mtoto wangu akafariki, niliumia sana; siku moja yule mganga alikuja kudai ile sehemu ya ardhi tuliyokubaliana kuwa akimponya mtoto wangu nitampa; wakati huo nikiwa na maumivu ya kumpoteza mtoto wangu, nilimfukuza kwa mapanga. Alipotea kwa kitambo kidogo siku moja wakaja maaskari na kunikamata na nikapewa kesi ya ubakaji ya kwamba nimembaka mke wa yule mganga, na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Nilihangaika sana kule gerezani mpaka nilipokutana na Wachungaji wa Efatha ndipo nikaamua kuokoka; baada ya kuokoka ndani ya miezi sita nikaachiwa huru, siku ya tarehe 3 mwezi huu wa 11 nikaachiwa huru.
Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania baada ya kuokoka mpaka sasa nipo huru na mimi nimeokoka. Hakika Mungu anaweza yote, mimi niliyekuwa mganga wa kienyeji lakini nilishindwa kujisaidia mwenyewe nilipokuwa kwenye matatizo lakini baada ya kukutana na Mungu kila kilichokuwa kinanitesa kimetoweka kwangu, nitamtumikia Mungu siku zote za uhai wangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*