Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mungu hufanya kazi na wampendao

NENO LA SIKU
Tarehe: 6/11/2023
Na Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira
Warumi 8:28 “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Je! Wewe unajua kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao? Wewe kama mwamini unapaswa kutambua hili na akili yako ilishike ili usife masikini. Watu wengi wameokoka wamembeba Yesu ndani yao lakini bado ni masikini, inawezekanaje? Kwa sababu ni wavivu wanapenda kupokea na sio kutenda.
Watendaji ni watenda kazi pamoja na Mungu, na kwa sababu ni watenda kazi ndio ambao Mungu anawatumia, kwa sababu hiyo Mungu anawastawisha, kwao hakuna umaskini. Kuwa maskini ni mtindo wa maisha na kuwa tajiri pia ni mtindo wa maisha ambao mtu anauchagua hivyo wewe ndiye unachagua ni mtindo upi wa maisha unautaka. Kuwa mtendaji pamoja na Mungu ili ule mema yake au uwe mvivu, kuwa mpanzi au kuwa mwenye njaa.
Mpanzi ni mtendakazi pamoja na Mungu, je! Wewe ni mpanzi au mlaji?.
Usipende kuwa mlaji bali kuwa mtendaji, kwa maana kwa jinsi unavyofanya kazi ya Mungu kamwe hatakuacha, atakuja kukuchukua na kukufanya uwe wake hivyo hautakuwa na ukata bali utakuwa na utele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*